Sunday, 13 January 2019

JINSI YA KUBADILISHA AINA YA FILE

 
Bila shaka zoezi hili wengi wa watu wamekuwa wakiwa na shauku nalo kulijua ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi. Katika hali ya kawaida file zote za music or video au picha au nyeninezo huwa na extension (aina) mbali mbali ambazo kila moja inafaida zake na hasara zake. 




Mfano wa aina hizo ni kama zifuatazo:


Audio:
 Mp3
 Wma
 Ape
 Flac
Wav 
Ogg 
M4r
 Amr na nyenginezo.

Video: 
 Mp4 
 Avi
3gp 
 Rmvb 
 Wmv 
 Mpeg 
 Mov na nyenginezo

Kwa vile ndio hanza tunaanza tutaangaza jinsi ya kubadilisha sauti au video kutoka type iliokuwa nayo kwenda nyengine ambayo sisi tunaitaka.
Njia na hatua ni hizihizi kama utakuwa mfatiliaji wa kweli naamini utafanikisha tu bila wasiwasi wowote lakini kumbuka kabla hatujaanza ‘Hakuna Kujifunza Kusiko na Majaribu’ hivyo kufanya majaribio ni suala ambalo litaongeza ujuzi wako.
Zana za kuwa nazo:
1- Microsoft Window (Xp , Vista, 2003, 7 na kuendelea)
2- Program iitwayo Format Factory
3- File yako ambayo utataka kuibadilisha aina yake.
Kwa sie hapa tutatumia file tulioipa jina la ‘mfano’.
Hatua za Kufuata:
Kwanza angalia file yako ni ya aina gani.
Nayo ni ku right click kisha kwenda katika properties utaona aina ya file yako.




Pili fungua progam ya Factory format
Tatu pembeni yako mkono wa kushoto utaona aina nyingi za file. Hapo utatakiwa kuchagua aina ambayo utataka baada ya kubadilisha iwe.


Katika jaribio letu sisi tutatumia mp3 kwa maana tunabadilisha kutoka mp4 kwenda mp3 ambayo nia audio tupu.
NB:
Kutakuwa kuna categories tofauti tofauti mfano kama inavyojionesha chini hapo sisi tumechagua audio lakini juu kuna video chini kuna piture, rom device\DVD\CD\ISO na advanced.

Chagua aina yako, baada ya kuchagua itakuleta kwenye sub window kwa ajili ya kuchagua file yako iliko pamoja na kuchagua location yako mpya kwa ajili ya file yako mpya.
Kisha utabonyeza Add file kwa ajili ya kutafta file yako, na kisha utabonyeza openi ili kuiruhusu iingie katika program yako.



Kisha utabonyeza OK ili kuanza kazi yetu.
Kisha utai highlight then utabonyeza start kwa kuanza kubadilisha aina ya file yako.
Inategemea na ukubwa wa file yako zipo ambazo huchukua mda mdogo kutokana na udogo wa file na ziko ambazo huchukua mda mwingi vivyo hivyo kulingana na ukubwa wa file.


Subiri mpaka ijiandike COMPLETED kuonesha ishara ya kuwa file yako kweli imeshakamlika kubadilishwa aina yake. Kwa kawaida file mpya itawekwa katika sehemu ileile yenye file ya zamani ili kurahisisha kuonekanwa.
Mfano wetu ulikua kwenye desktop hivyo file yetu itakaa kwenye desktop vile vile.
Hebu tuiangaze file yetu mpya imebadilika aina au laa.

Yes tumefanikiwa kwenye kubadili aina ya file kutoka namna moja kwenda nyengine.
Usikose kufatilia kwa kuwa darasa ijayo tutajadili jinsi ya kubadilisha picha kutoka aina moja kwenda aina nyenine
Kwa masuali, ushauri, maoni, pamoja na kutaka msaada usisite kuwasiliana nami kupitia

Ahsanteni.
Usiwe Mchoyo Wape na Wenzako Wanufaike.
 


0 comments :

Post a Comment

Popular Posts

Blog Archive

mbdully. Powered by Blogger.